Mazingira FM

Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bunda walia na mpango wa wanufaika wa TASAF kufanyishwa shughuli za kulima barabara.

4 March 2023, 6:57 pm

Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara walia na mpango wa wanufaika wa TASAF kufanyishwa shughuli za kulima barabara ndipo wapewe fedha zao.

Wakizungumza katika Baraza la Madiwani mkutano wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 uliofanyika tarehe 2 March 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri madiwahi hao wameitaka serikali kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo ambalo limeelezwa kulalamikiwa na wananchi wao.

SAUTI ZA MADIWANI

Akitoa ufafanuzi wa suala hilo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji wa Bunda, Emmanuel Mkongo amesema ni utaratibu mpya ulioanzishwa na Tasaf kwa lengo la kuwaidia walengwa kujua kwamba kuna kufanyakazi na kwamba hutapata hela hiyo hadi ufanye kazi.

MKURUGENZI EMMANUEL MKONGO