Mazingira FM

Wakaazi wa Nyamuswa walalamika kuingiliwa kingono kwa njia za kishirikina

3 March 2023, 2:05 pm

Wakaazi wa Kijiji Cha Nyamuswa Kata ya Nyamuswa Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara

Wakaazi wa Kijiji Cha Nyamuswa Kata ya Nyamuswa Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara wamelalamikia vitendo vya kuingiliwa kingono wakati wamelala jambo linaloleta taharuki kwa wananchi

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema licha ya vitendo hivyo kukemewa na viongozi wa kata kupitia mikutano lakini bado hali hiyo inaendelea.

Wakazi hao wameongeza kuwa Kuna Mwananchi mwingine anawadanganya wanafunzi kwa pipi na miwa ambayo wanaamini inausishwa na mambo ya kishirikina ili kuwabaka.

Sauti ya Miss Walioba akizungumza

Wananchi wa Kata ya Nyabitele na Ramboni wamelalamikia suala la kuingiliwa kingono wakati wamelala Kwa njia ya kishirikina

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamuswa

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyamuswa Mhe Ibrahim Mganga amesema ni kweli tatizo hilo lipo kwenye vitongoji viwili ndani ya kata yake ambavyo ni nyabitele na Ramboni wananchi wamekuwa wakilalamikia suala la kuingiliwa kingono wakati wamelala Kwa njia ya kishirikina na waliitisha kikao na kukemea suala hilo lakini bado malalamiko bado yapo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Nyamuswa Mhe Ibrahim Mganga

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano amesema jambo hilo halikubaliki na amewataka wakaazi wa Nyamuswa wawe watulivu wakati ofisi ya mkuu wa wilaya ikilifanyia kazi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano