Mazingira FM

RUWASA Bunda; Ifikapo 2025 Bunda kupata maji 85% vijijini

1 March 2023, 4:38 pm

Meneja wa RUWASA wilaya ya Bunda Mhandisi William Boniphas amesema ifikapo 2025 wilaya ya Bunda itakuwa imefikia 85% ya upatikanaji wa maji vijijini kama inavyoelekeza ilani ya CCM ya 2020 na 2025

Hayo ameyasema ofisini kwake wakati akizungumza na Mazingira FM iliyofika kutaka kujua maendeleo ya miradi ya maji na changamoto za wananchi namna wanavyozitatua za upatikanaji wa maji katika maeneo yao.

Mhandisi Boniphas amesema kwa sasa RUWASA wanatekeleza miradi kadhaa kama vile miradi ya UVICO-19 ambapo RUWASA Bunda walipokea shilingi 1.5 bilioni kukamilisha miradi ya Sanzate, Bitaraguru na Mugara – Nyarugoma, ambapo kwa Bunda wanahudumia vijiji 78 na mitaa 10 huku ikiwa imewafikia wananchi 273,000 sawa na asilimia 71.6%

Aidha Mhandisi Boniphas amesema mradi wa maji Mcharo ipo hatua ya mwisho kawa kuwa suala la umeme ndo alijakamilika lakini wamewasiliana na TANESCO kuona namna wanavyoweza kulitatua kwa haraka kwa maana kwa upande wa RUWASA kila kitu kipo kuanzia kwenye ujenzi wa DP mota na pampu kilakitu kipo tayari hivyo wakazi wa mcharo muda wowote watapata maji TANESCO wakimaliza kuunganisha mfumo wa umeme.