Mazingira FM

Jamii imeaswa kusikiliza vyombo vya habari ili kuimarisha matumizi ya Kiswahili

26 February 2023, 11:30 am

Jamii imeaswa kuendelea kusikiliza vyombo vya habari ili kujiimarisha zaidi katika matumizi ya lugha ya kiswahili na kuifanya lugha hiyo iendelee kukua na kuenea katika maeneo mbalimbali duniani.

Wito huo umetolewa leo tarehe 24 FeB 2023 kupitia Ziara ya Wanafunzi wa Kidato cha 4 Shule ya Sekondari Kunzugu iliyopo Halmashauri ya Mji Bunda Mkoani Mara wakati walipofika studio za Radio Mazingira Fm kwa lengo la kujifunza mchango wa vyombo vya habari katika kukuza na kueneza lugha ya kiswahili.

Aidha wanafunzi wameupongeza uongozi wa Radio Mazingira Fm kwa mapokezi yao na kuwapa nafasi ya kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho katika utoaji wa habari na kuendelea kuielimisha jamii.

Katika ziara hiyo iliyowahusisha wanafunzi 120 waliweza kutembelea sehemu mbalimbali za kituo hicho ikiwa ni pamoja na vyumba vya uchakataji na uandaaji wa habari pamoja na chumba cha urushaji wa matangazo.