Mazingira FM

Sitaki niongoze wilaya ya watu wenye njaa : DC Bunda

23 February 2023, 9:24 pm

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano amesema hataki kuongoza Wilaya ambayo watu wake Wana njaa

Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao Cha Baraza maalumu la madiwani lililoketi Juma hili kulijadili zoezi la Nyatwali

Amesema katika maeneo mengi ya Wilaya ya Bunda wakulima waliolima mahindi hayana hali nzuri lakini waliolima Mtama una hali nzuri hivyo kuwataka wananchi wa Bunda walau kila kaya iwe na ekari moja ya Mtama ili kupunguza tatizo na hatari ya njaa

Aidha katika hatua nyingine Mhe Dkt Naano amesema tatizo la utoro  shuleni na mimba kwa wanafunzi bado nichangamoto kwa Wilaya ya Bunda jambo linalopelekea matokeo mabaya katika mitihani