Mazingira FM

Ajali ya basi la Afrika Raha dereva alikuwa ‘bize’ na simu

16 February 2023, 12:36 pm

Mwendokasi na dereva kuwa ‘bize’ na simu wakati wa safari ni chanzo cha ajali ya Basi la Afrika Raha iliyotokea siku ya jumapili tarehe 12 Feb 2023 eneo la Mwibagi Wilaya ya Butiama mkoa wa Mara barabara ya Mwanza Musoma.

Marwa Gisire Kekaryo ni mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo ambaye alikuwa amekaa karibu na dereva amesema “dereva alikuwa ‘spidi’ sana halafu muda mwingi anaongea na simu nilipojaribu kumwambia akasema njoo uendeshe wewe”

Marwa anasimulia kuwa dakika chache kabla ya ajali hiyo alimuona dereva anaongea na simu kisha akacheka hadi akainama chini na alipogeuza macho kuangalia mbele ndipo alipojikuta anahangaika kuikwepa gari iliyokuwa inakuja mbele yake ndipo walipopinduka na gari.

Hii imethibitishwa na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akizungumza na Radio Mazingira Fm kwa njia ya simu juu ya tukio hilo iliyolihusisha basi la Afrika Raha lenye Namba T382 DSL Aina ya ASIA STAR mali ya Sylvester Wambura Ogondo