Mazingira FM

Aliyepambana na mamba kwa dakika 15 majini asimulia alivyonusurika

16 February 2023, 12:31 pm

Boniface Nkwande mkazi wa Buzimbwe aliyepambana na Mamba kunusuru maisha yake

Boniface Nkwande mkazi wa Buzimbwe kata ya Bulamba Halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya DDH Bunda baada ya kushambuliwa na mamba na kujeruhiwa mkono wake wa kulia.

Akisimulia tukio hilo amesema lilitokea jumamosi tarehe 11 Feb 2023 majira ya saa moja jioni wakati akiwa anaoga kandokando ya ziwa victoria katika eneo la Buzimbwe ghafla mamba alitokea na kumkamata mkono wa kulia na kumvutia ndani ya maji.

Amesema katika juhudi za kujinasua alijigeuza na kupanda mgongoni mwa mamba na kujaribu kuomba msaada ambapo kuna watu walikuja na mtumbwi na kumvuta kutoka katika kinywa cha mamba