Mazingira FM

Mazingira FM yaadhimisha Siku ya Radio Duniani kwa bonanza kubwa Bunda

14 February 2023, 8:02 am

Wananchi wa Bunda waliojitokeza kwenye Bonanza la Mazingira Fm Maadhimisho ya siku ya Radio Duniani uwanja wa sabasaba.

Katika kusherekea siku ya radio Duniani Mazingira fm imefanya Bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukimbiza kuku ,kukimbia na yai kwenye kijiko, mchezo wa bao na mpira wa miguu, ikiambatana na utoaji wa elimu na chanjo ya uviko-19 Kwa wananchi wa wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Akitoa Elimu ya chanjo ya uviko – 19 mganga mkuu wa Hospitali Manyamanyama Dkt.Isack James, ametoa wito Kwa jamii kuendelea kujikinga na uviko -19 hususani Kwa kupata chanjo na kuzingatia Yale yote yanayoelekezwa na wataalam wa afya.

Wakaazi wa Bunda wakisikiliza mtaalamu wa Afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa Uvico-19

Bonanza Hilo limefanyika Feb 12,2023 katika uwanja wa sabasaba Bunda Mjini ikiwa ni siku moja kuelekea maadhimisho ya Siku ya radio Duniani ambayo uadhimishwa kila tarehe 13 Feb kila mwaka huku kauli Mbiu ya mwaka huu ni Radio na Amani

Aidha meneja wa kituo Cha radio Mazingira Fm Ally Nyamkinda amekabidhi zawadi ya mbuzi na kreti la soda Kwa washindi wa mpira wa miguu ambao ni Bajaji FC waliokua wakicheza na Bodaboda FC ambapo Bajaji waliibuka washindi kupitia changamoto za mikwaju ya penati ambapo walishinda penarti 4 kwa 3, dhidi bodaboda huku mechi nyingine ikiwa Kati ya Mazingira Fm dhidi ya CRDB bank ambapo Mazingira fm waliibuka kwa ushindi wa bao 2 – 0
Sambamba na hilo Meneja Ally Nyamkinda alimkabidhi zawadi ya pesa gorikipa wa timu ya Bajaji Kwa kazi nzuri alioifanya.

Meneja wa Radio Mazingira Fm akifurahia baada ya kukabidhi zawadi kwa timu ya Bajaji baada ya kuibuka washindi dhidi ya bodaboda

“Naomba gorikipa wa timu ya Bajaji aje hapa, hesabu ya bosi ya leo nampa mimi,na nakabidhi zawadi hii ya mbuzi na cleti la soda Kwa timu ya Bajaji na hongereni Kwa ushindi” amesema Nyamkinda
Naye mwenyekiti wa kamati ya Bonanza Hilo Thomas Masalu alikabidhizawadi Kwa washindi watatu wa mchezo wa bao ,huku mshindi wa kwanza akipewa Tsh.15000, mshindi wapili akipewa Tsh 10000 na mshindi wa tatu Tsh.5000.

Hata hivyo Bonanza Hilo liliambatana na uzinduzi wa mchakato wa kumsaka mtoto mwenye kipaji Cha utangazaji ambae atapata nafasi ya kutangaza kipindi Cha watoto Radio Mazingira Fm iliopo Wilayani Bunda mkoani Mara.

Redio inatazamwa kama chombo muhimu na sehemu muhimu ya kutunza amani. Redio hushughulikia visababishi na vichochezi vya migogoro, kabla hazijaweza kulipuka na kuwa vurugu.

Inatoa mbinu mbadala ya kuzuia migogoro, au migongano ya maslahi, kuondoa kutoelewana, na kutambua masuala ya kutoaminiana.

Hii inaweza kusaidia kukabiliana na chuki, hamu ya kulipiza kisasi, au nia ya kutumia silaha.

Na Catherine Msafiri