Mazingira FM

Bunda: Wazazi wafundisheni watoto kuridhika ili muepushe mimba za utotoni

11 February 2023, 7:11 pm

Pili Bakari Afisa Ushirikiano kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la kuunganisha Uwezo na Maendeleo ya Jamii ICCAO Tanzania,

Wazazi na walezi wametakiwa kuwafundisha watoto waridhike na kile walichonacho ili kuwaepusha na vishawishi vinavyopelekea mimba za utotoni na kukatisha ndoto zao.Wito huo umetolewa jana tarehe 8 Feb 2023 na Afisa Ushirikiano kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la kuunganisha Uwezo na Maendeleo ya Jamii ICCAO Tanzania, Pili Bakari wakati akizungumza na viongozi pamoja na wakazi wa kata ya Kabarimu Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara kupitia mradi wa Asome wenye lengo la kupiga vita mila potofu zinazosababisha kukatisha masomo. Pilli amesema watoto wengi wanakumbana na changamoto mbalimbali za mimba na ndoa za utotoni huku sababu kubwa wanayokuwa wakiieleza ni kutokana na umasikini na ugumu wa maisha hivyo amewataka wazazi kujitahidi kuwafundisha watoto kujua umuhimu wa shule katika kutimiza malengo yao.

Aidha wazazi na viongozi kutoka kata ya Kabarimu wamekuwa na maoni mseto katika namna ya kupambana na changamoto ya wananfunzi kubeba ujauzito na kukwamisha ndoto zao za kuendelea namasomo

By Edward Lucas