Mazingira FM

Jumuiya Ya Wazazi Ccm Bunda Yaadhimisha Miaka 46 Ya Ccm; Yasema Haijalidhishwa Na Ujenzi Wa Choo Kituo Cha Afya Mugeta.

27 January 2023, 8:25 pm

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Bunda Ndugu Leonard Magwayega amesema hajalidhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa choo na jengo lakufulia kituo Cha Afya Cha Mugeta kilichopo kata ya Mugeta Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Ndugu Magwayega ameyasema hayo katika ziara ya kuadhimisha miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kwa jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bunda yamefanyika kata ya Mugeta

Aidha mwenyekiti huyo amesema mnamo tarehe 19 mwezi huu kamati ya siasa ya Wilaya Chini ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ilifika kwenye kituo hicho katika kukagua utekelezaji wa ilani na kutoa maelekezo jambo la kushangaza hadi Leo hakuna kilichofanyika.

” Nashangaa tarehe 19 tulifika hapa tukakuta mambo ya ajabu hapa kuna choo tangu mwaka 20 serikali ilitoa fedha milion 22 lakini hadi Leo hakijakamilika na yalitolewa maelekezo kufika tarehe 31 mwezi huu choo hicho kiwe kimekamilika lakini hadi Leo hakuna kilichofanyika hili jambo halikubaliki”

Kwa upande wake Nganga wa zamu katika kituo hicho jina limeifadhiwa kwa niaba ya mganga mfawidhi amesema katika kituo hicho zipo changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa wodi ya wagonjwa, mipira ya mkojo kwa akina mama wanaojifungua, mabomba ya sindano pamoja na mipira ya drip ambayo zaidi ya miezi minne haipo hospitalini hapo