Mazingira FM

CCM Bunda; yapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani yampa hati ya pongezi mkuu wa wilaya Nassar aliyehamishwa siku ya kuwasilisha taarifa

27 January 2023, 7:53 pm

Halmashauri kuu ccm wilaya ya bunda chini ya mwenyekiti wa chama hicho ndugu pius magese mayaya imepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa mwaka 2022.

Akiwasilisha taarifa hiyo mhe mkuu wa wilaya ya bunda mhe Joshua Nassar amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya ya Bunda katika sekta za Elimu, Afya, Barabara, Maji,  Umeme miongoni mwa sekta zingine.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda ndugu Mayaya amesema wameridhishwa na utekelezaji wa kazi za maendeleo ndani ya wilaya ya Bunda baada ya kamati ya siasa ya wilaya kupita na kukagua miradi takribani 42 ndani ya wilaya ya Bunda.

Pamoja na pongezi hizo mwenyeti wa CCM ameitaka serikali kushughulikia changamoto zilizobainika katika ziara ya kamati ya siasa ikiwemo upungufu wa madawati na uchakavu wa madarasa katika  shule za msingi hasa zile kongwe.

Ikubukwe Mhe Nassar ni miongoni mwa wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vyao vya kazi akihamishiwa wilaya ya Iramba mkoani Singida.