Mazingira FM

BUWASA; wanaojiunganishia maji Bunda kukiona.

January 25, 2023, 7:49 am

Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda imewaonya wananchi wanaojiunganishia maji kinyemela bila taarifa ya mamlaka kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa  dhidi yao pindi watakapobainika

Hayo yamesemwa na Moyo Faya kutoka Mamlaka ya maji Bunda wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji kwa wateja ambapo imebahatika kumkamata mteja mmoja aliyejiunganishia maji na kuisababishia mamlaka hasara

Moyo Amesema mteja waliyemkamata leo eneo la CN Bunda mjini kwa siku alikuwa akitumia unit 28 za maji ambazo zilikuwa hazipiti kwenye mita.

Mwanasheria wa mamlaka ya maji Bunda bi Belnadeta Lugendo amesema ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kujiunganishia maji na adhabu yake ni kuanzia laki tano hadi shilingi milioni hamsini au kifungo jela au vyote kwa pamoja kadri mahakama itakavyotoa hukumu ya kesi husika