Mazingira FM

Mkurugenzi Mazingira FM akabidhi msaada kwa mtoto mwenye ulemavu

January 23, 2023, 4:30 pm

Mkurugenzi wa radio Mazingira Fm ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ketale Mhe Mramba Simba Nyamkinda amemkabidhi baiskeli ya magurudumu mawili kwa bi Ferda Wanjara mkazi wa kata ya Nyasura ambaye ni mama mzazi wa mtoto Elizabeth John mwenye ulemavu wa viungo.

Sambamba na makabidhiano hayo yaliofanyika leo katika ofisi za radio mazingira fm ,Mheshimiwa Mramba amesema kupitia kipindi kilichorushwa radio mazingira kuhusu mama huyu akiomba  msaada aliahidi kumsaidia na leo ametimiza ahadi yake.      

Nae ferda wanjara ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo ametoa shukrani zake na kuendelea kuwaomba wanajamii kuendelea kumsaidia mtoto wake kwani hata nguo za shule hana.

Aidha diwani  wa kata ya Nyasura Magigi Samweli Kiboko amemshukru Diwani Mramba na uongozi wa radio mazingira kwa msaada kwa mtoto huyo huku akiwaomba watu wenye watoto wenye ulemavu wasiwafiche ndani.

Itakumbukwa ferda  wanjara na mwanae walifanya mahojiano tarehe kumi na tisa mwezi wa tisa mwaka 2022 kupitia kipindi cha sema usikike kinachorushwa radio mazingira fm kila siku ya jumamosi kuanzia saa sita na robo.