Mazingira FM

MCH MOTOMOTO, Wasaidieni Yatima maana hujui kesho watakuwa nani.

22 January 2023, 9:10 pm

Wito umetolewa kwenye jamii kuwahudumia watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu kwa kuwa hawakutaka kuwa hivyo

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto wakati wa harambee ya kutafuta fedha ya ununuzi wa kiwanja Cha kujenga kituo Cha watoto Yatima.

Harambee hiyo imeendeshwa na kanisa la levaival Buptist Nyasura Chini ya mchungaji kiongonzi Jeremiah Motomoto ambapo wanalengo la kupata shilingi milioni 75 ili kununua ekari 10 ili kujenga kituo hicho.

Mhe Maboto aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo amesema kwa nafasi yake kama mbunge na Mkurugenzi wa Kampuni ya Maboto microfinance ameahidi kushirikiana na mchungaji Motomoto ili kuhakikisha kituo hicho kinajengwa ambapo katika harambee hiyo ametoa kiasi Cha shilingi mil 1.5.

Naye Diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samwel Kiboko ameshukuru kanisa la Baptist Nyasura kwa kuona umuhimu wa watoto Yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu.

Kwa upande wao mfuko wa maendeleo wa Wachungaji Mkoa wa Mara ma Kikundi Cha Wachungaji Bunda wameshukuru maono ya mchungaji Motomoto ya kuwakumbuka wahitaji maana hiyo ndiyo dini ya kweli.

Naye mchungaji wa kanisa hilo Jeremiah Motomoto amesema ni wajibu wa jamii kuwasaidia watoto yatima kwa kuwa hujui atakuwa nani kesho