Mazingira FM

DAS BUNDA: kiongozi wa AMCOS atakayekiuka kiapo chake sheria itachukua mkondo wake

January 18, 2023, 8:01 am

 

 

Katibu tawala wilaya ya bunda mhe Salum Halfan Mterela amewataka AMCOS wilayani Bunda kuzingatia uadilifu na maadili katika kazi yao ili kulinda viapo vyao.

 

Hayo ameyasema wakati wa uapisho wa viongozi wa AMCOS wilaya ya Bunda ambapo takribani viongozi 158 ambao ni wenyeviti na makatibu wa AMCOS wameapishwa ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika tukio hilo huku sababu ikitajwa kuwa ni vitendo vya ubadhirifu vilivyozoeleka kufanywa na viongozi hao wakati wakitekeleza majukumu yao.

Mterela amesema ni wakati sasa AMCOS  kubadilika kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika kama vile wizi wa pembejeo, kuwaibia wakulima pamba yao kupitia mizani pamoja na changamoto zingine

Kwa upande wake wake Hemed Kabea ambaye ni mkaguzi wa zao la pamba wilaya ya Bunda kutoka bodi ya pamba Tanzania amesema serikali kupitia bodi ya pamba imekuja na mpango huo wa kuwaapisha viongozi wa  hao baada ya kuwepo changamoto lukuki katika AMCOS nyingi nchini za wizi na ubadhilifu wa pembejeo ikiwemo viuatirifu na fedha ya wakulima hivyo njia hii itajenga woga kwa viongozi hao kiujihusisha na wizi wa aina yoyote.