Mazingira FM

Mbunge wa Bunda Mjini Mhe Robert : apokea kero kutoka kwenye kata 14 za Bunda Mjini huku maji na barabara vikichukua nafasi

15 January 2023, 5:53 pm

  • Mbunge Wa Jimbo La Bunda Mjini Mhe. Chacha Robart Maboto amefanya Mkutano Na Viongozi Wa Chama Cha Mapinduzi Wenyeviti Wa Kata,Makatibu Kata, Wenezi Kata Pamoja Na Madiwani Viti Maalum Kupitia Kata Zote 14 Zinazounda Jimbo La Bunda Mjini.

Mkutano Huo Umefanyika Katika Ukumbi Wa Heliet Mjini Bunda Lengo Ikiwa Ni Kupokea Changamoto Wanazo Kumbana Nazo Wananchi Wa Jimbo La Bunda Mjini Na Kata Zake, Ambapo Viongozi Hao Wametoa Kero Mbalimbali za Kata Zao ,Huku Kero Kubwa Ikiwa Ni miundombinu mibovu ya Barabara Za Mita kama vile Makaravati,Mitalo Pamoja maji.

Akijibu Hoja Na Kero Za Viongozi Mbalimbali Wa Chama Cha Mapinduzi Kata Pamoja Na Madiwani Mhe. Chacha Maboto Amesema ni jumkumu la kiongozi kupeleka maendeleo kwa wamanchi na kuisimamia vizuri.

Kwa Upande Mwingine Mbunge Chacha Maboto Kupitia Mfuko Wa Jimbo Na Mshahara Wake wa ubunge Ameelezea namna ambavyo ameweza kugusa sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kusomesha Watoto Walio Katika Mazingira Magumu, Ambapo amehaidi kusaidia Wanafunzi Hao Mpaka Pale Ubunge wake Utakapo Koma.

Aidha kupitia kampuni ya maboto microfinance LTD, ambayo mhe. Mbunge ndiye mkurugenzi wake Imeanzisha program maalum ya kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu katika elimu, kwa kuwasomesha na kuwapatia vifaaa muhimu vya kitaalum,Ambapo kwa kwa mwaka huu wa 2023 wameanza kwa kutoa msaada huo kwa watoto 14 wenye thamani ya shilingi milioni 2.