Mazingira FM

Mbunge Getere; awapongeza Nyaburundu kujenga shule ya Sekomdari

15 January 2023, 5:32 pm

Mbunge wa jimbo la Bunda mh. Bonphace Mwita Getere amewapongeza wanakijiji cha Nyaburundu kata ya Ketare kwa nia njema waliyoonesha ya kujega Shule ya Sekondari katika kijiji hicho.

Mh. Getere ameyasema hayo katika ziara yake jimboni wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyaburundu.

Amesema yeye kama mbunge atahakikisha shule hiyo inakamilika ndani ya mwaka huu ili mwakani wanafunzi waanze kusoma katika sekonadari hiyo.

Kwa upande wake afisa elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Bunda mwl Wandere Lwakatare amesema kuwa ujenzi wa shule ya sekondari sio kuweka chumba kimoja bali kuna vipengele vingi vinaangaliwa kabla ya  kusajili shule