Mazingira FM

Bunda; Sasa rasmi wakazi wa kata ya Nyatwali kuhama serikali yasema

5 January 2023, 8:54 am

Serikali imetangaza adhima yake kuhusu kulitwaa eneo la kata ya  Nyatwali lililopo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara kuwa sehemu ya hifadhi ya taifa ya Serengeti

Kamati ya mawaziri nane wa kisekta wakiongozwa na mwenyekiti wao ambaye pia ni waziri wa aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dr Angelina Mabula imefika katika kata hiyo ya Nyatwali na kuzungumza na wananchi juu ya adhima hiyo ya serikali ya kulitwaa eneo la nyatwali

Akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyatwali Mhe waziri Mabula amesema serikali imeamua kulichukua eneo la Nyatwali kwa lengo la kulinda maslai ya umma na wana Nyatwali kwa ujumla

Mapema akizungumza na wakazi kwenye mkutanoo huo Mhe Mary Masanja naibu waziri wa Maliasili na utalii amesema eneo la Nyatwali tangu mwanzo lilikuwa ni pori tengefu ambapo kisheria wananchi wanaweza kufanya shughuli zao lakini kutokana na mikataba ya kimataifa juu ya uhifadhi hasa hifadhi ya taifa ya Serengeti hawanabudi kuliachia eneo hilo

Kwa upande wao wakazi wa Nyatwali wameiomba serikali kuzingatia maslahi yao ya namna bora ya kuamishwa na kuzingatia stahiki zao pindi wanapofanyiwa tathimini ya maeneo yao

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Mabotto amesema Nyatwali ni moja ya kata 14 zilizopo ndani ya jimbo lake na wakazi wa Nyatwali hawajakataa mpango wa serikali kuwaamishi ila wanachokiitaji ni elimu juu ya kuama kwao

 

Aidha Mhe Mabotto ameitaka serikali kuwaambia wananchi wa kata ya Nyatwali juu ya kama wanahama wanaenda wapi? Utaratibu gani unatumika kuwaamisha? Yale waliyokuwa wanayapata Nyatwali huko waendako watayapaje?

“ naishauri serikali iwaambie watu hawa kwa sababu ndiyo wahanga wa zoezi la kuhamishwa namna ya zoezi lilivyo na mtazingatiaje maslahi yao pia elimu ya kina itolewe kwao”

 

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo Mhe Joshua Nassar amesema zoezi linaendelea vizuri na Hadi sasa wamefikia hatua ya utathmini ambapo Hadi sasa wamefanya tathmini huku vikao 12 vikiwa vimefanyika vya utoaji wa Elimu.