Mazingira FM

Umoja wa Kikundi Cha Wachungaji Bunda wametoa msaada wa chakula (mahindi ) magunia 10 kwa watoto 75 wanaoishi Mazingira magumu.

1 January 2023, 6:43 pm

Umoja wa Kikundi Cha Wachungaji Bunda wametoa msaada wa chakula (mahindi ) magunia 10 kwa watoto 75 wanaoishi Mazingira magumu.

Msaada huo umetolewa 31 Dec 2022 katika kanisa la FPCT sabasaba Bunda mjini na kuudhiriwa na viongozi wa kiserikali huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salum Halfan Mterela kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassar.

Mwenyekiti wa Umoja huo mchungaji Elikana Magigita Amesema wao kama viongozi wa kiroho wamewiwa kutoa sadaka hiyo kwa wahitaji huku akiishukuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye madhebu ya dini

Kupitia risala ya Wachungaji hao iliyosomwa na mchungaji Omoso mbele ya mgeni rasmi imebainisha changamoto ya mahitaji Muhimu kwa familia ambazo hazijiwezi

Amesema Kikundi hicho kimeanzishwa mwaka 2017 kwa Wachungaji wenye hiari huku kikiwa na malengo ya kumsaidia mchungaji katika Shida na raha, katika ujenzi wa nyumba za ibada na kumsaidia mchungaji kiuchumi.

Katika risala hiyo mchungaji Omoso amesema umoja wa Wachungaji hao umeandaa magunia kumi ya mahindi ambayo yamepatikana ndani na nje ya umoja huo na kila mtoto anapata kilo 12 za mahindi

Kwa niaba ya mkuu wa Wilaya Mhe katibu tawala Wilaya ya Bunda Salum Halfan Mterela amesema ni jambo la baraka kuwakumbuka wahitaji maana ndivyo maandiko yameagiza na ameahidi kutoa shilingi laki Tano ili msaada huo uwe endelevu kwa wahitaji.

Kwa upande wao waliopokea msaada huo wamewashukuru viongozi hao wa dini kwa kuona umuhimu wa kuwapa msaada huo maana utawasaidia kutatua changamoto ya chakula katika familia zao.