Mazingira FM

MAZINGIRA FM kutanua masafa 2023

1 January 2023, 5:57 pm

Ally Nyamkinda Meneja Mazingira Fm

Meneja wa kituo cha utangazaji cha radio Mazingira Fm Ally Simba Nyamkinda  amewashukuru wasikilizaji na wadau wote wa Redio Mazingira kwa mwaka 2022 huku akibainisha kuwa Mazingira Fm ipo kwa ajili yao.

Hayo ameyasema  katika mahojiano na kipindin cha Asubuhi leo ambapo amesema mtangazaji hawezi kuamka asubuhi kutangaza kitu kutoka kichwani mwake badala yake ni kile anachokiitaji msikilizaji na kuzingatia sheria na miongozo ya utangazaji

“mimi binafsi na msimamo wa kituo hatuwezi kuamka asubuhi tukaanza kutangaza kitu kutoka kichwani badala yake ni vile wasikilizaji wetu wanataka  mfano kwenye kipindi cha asubuhi leo kuna kipengere cha Chai ya Asubuhi maoni ya wasikilizaji ni mengi juu ya kuongezewa muda pia kufanyika mara mbili kwa vsiku tutalifikilia lakini sisi redio mazingira hatutafanya vipindi kwa kufuata wengine mimi kama msimamizi wa kituo nilisema sheria, kanuni na taratibu za mamlaka ya mawasiliano tanzania kwa asilimia 100%” alisisitiza Ally.

Aidha amewataka wasikilizaji wote kuendelea kuifuatilia Mazingira Fm kwa mwaka 2023 kwa kuwa saizi inapatikana kupitia masafa tofauti ikiwemo Fm,  91.7Mhzmtandao   Radiotadio.co.tz/mazimgirafm

na setelaiti  Eutelsat 5 .