Mazingira FM

Bunda: Joyce Mang’o (MNEC) kupitia UWT afungua mafunzo ya uongozi UWT Bunda Mjini

20 December 2022, 6:16 pm

 

Mjumbe wa halmashauri kuu ccm taifa kutoka UWT ndugu Joyce Mang’o amefungua mafunzo ya umoja wa wanawake chama cha mapinduzi(UWT) jimbo la bunda mjini iliyowahusisha wenyeviti na makatibu wa (UWT) ngazi ya matawi , kata na viongozi ngazi ya wilaya.

Akizungumza katika ufunguzi huo leo 20 Dec 2022 Joyce amewataka wanawake kuwa na ushirikiano katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo, kupinga ubaguzi miongoni mwa wanawake, kushiriki katika shughuli za maendeleo bila kuchoka.

Amesema hakuna maendeleo pasipokuwashirikisha wanawake kwa kuwa wanao mchango mkubwa kwenye jamii na chama akitolea mfano usemi usemao.

‘’ukitaka kufika mbali nenda mwenyewe ila ukitaka kwenda mbali zaidi nenda na wenzako’’, pia usemi usemao ‘’ukitaka jambo lizungumzwe vizuri mwambie mwanaume ila ukitaka jambo lifanyike vizuri mwambie mwanamke’’.

‘’Wanawake tuna kazi kubwa ya kufanya tuache kubaguana, tuache makundi tutasonga mbele baada ya kumaliza uchaguzi ngazi ya chama tunaelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na serikali kuu siyo mbali tunakazi kubwa yakufanya kama wanawake’’.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduzi wilaya ya bunda ndugu Marysiana Sabuni amesema lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wanawake ambao wamechaguliwa katika chaguzi za CCM ndani ya wilaya ya bunda na kwa sasa wameanza na jimbo la bunda mjini.

‘‘tunataka wanawake waliochaguliwa wajue wajibu wao na majukumu yao tumeandaa mafunzo haya tukiwalenga wenyeviti na makatibu wa UWT kuanzia ngazi ya matawi kata na viongozi wa UWT wilaya tunataka tuwe na wanawake amabao hawana kigugumizi katika kutekeleza majukumu yao’’.

Naye katibu wa UWT Wilaya ya Bunda Evodia Zumba amesema suala la kuwajengea uwezo viongozi wa Chama hasa kwa upande wa jumuiya ya UWT ni ya kikanuni isipokuwa viongozi walikuwa na mazoea ya kutokufanya mafunzo.

Zumba ameongeza kuwa maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr. Samia Suluhu Hasani katika mkutano mkuu wa Chama kwamba yafanyike mafunzo kwa viongozi ngazi ya matawi, Kata, Wilaya, mikoa mpaka Taifa ili viongozi watambue wajibu wao.

Seminana hii ya mafunzo ya uongozi nakutambua majukumu yao inawajumbe 176 kutoka katika jimbo la bunda mjini.