Mazingira FM

BUFADESO BUNDA: wafanya mkutano mkuu wa shirika

17 December 2022, 2:46 pm

Shirika la BUFADESO linalojihusisha na utoaji elimu kwa jamii juu ya masuala ya kijinsi na kuwajengea uwezo wakulima mkoani mara limefanya mkutano mkuu wa mwaka ambapo imepokea taarifa mbalimbali zilizofanywa na shirika hilo kwa mwaka wa 2022.

Akitoa taarifa ya shirika hilo mratibu wa bufadeso Baraka Kamese amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2022 shirika hilo limeweza kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uiamalishaji na uendelezaji wa vikundi, ujasiriamali, utunzaji wa mazingira miongoni mwa mambo mengine.

Kwa upande wa taarifa ya fedha iliyowasilishwa na Marwa Nyamhanga mweka hazina kutoka BUFADESO amesema jumla ya shilingi million 10 zimetumika katika utekelezaji wa mambo mbalimbali katika shirika hilo ikiwemo ujenzi wa ofisi katika kata ya Kunzugu mtaa wa Ichamo ambao ujenzi bado unaendelea, ujenzi wa choo, tangu mwaka 2018 fedha iliyotokana na michango ya wanachama.

Kwa upande wake kwa niaba ya mgeni rasmi diwani wa kata ya Nyamakokoto Mhe Emmanuel Malibwa amewataka viongozi na wanachama wa BUFADESO kuendelea kutunza mazingira pia kushirikiana na viongozi kutatua changamoto zinazowakabili kama shirika.