Mazingira FM

Bunda: halmashauri kuu ccm bunda stoo wapokea taarifa ya utekerezaji wa ilani 2022

16 December 2022, 8:46 am

Halmashauri kuu ya ccm kata ya bunda stoo ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Charles Mwita Chacha imepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa mwaka 2022

Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu hiyo leo 15 Dec 2022 afisa mtendaji wa kata ya Bunda stoo Kasika Philemoni Thomas amesema kata hiyo imepokea fedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya elimu, afya, barabara miongoni mwa miradi mingine.

Kwa upande wao wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm kata ya bunda stoo wakiongozwa na mwenyekiti wao wamempongeza diwani na viongozi wengine kwa kuendelea kuleta miradi ya maendeleo huku wakigusia tatizo la barabara za mitaa, uchakavu wa shule ya msingi migungani na suala la dampo kama changamoto katika kata hiyo.

Naye diwani wa kata hiyo flavian chacha nyamigeko amesema changamoto zilizoainishwa na wajumbe wa halmashauri nhiyo ya chama ikiwemo ubovu wa barabara katika baadhi ya maeneo suala la dampo atakwenda kushirikiana na viongozi wengine akiwemo mbunge kuweza kuyatatua