Mazingira FM

Mafunzo ya risk management kwa watumishi wa halmashauri ya mji wa bunda

14 December 2022, 6:50 pm

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Adelina Mfikwa Leo tarehe 13.12.2022 amefungua mafunzo ya siku mbili ya Risk Management kwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kutoka katika kila Idara na Vitengo.

Bi. Adelina amewataka Watumishi hao kuzingatia na kuelewa vizuri mafunzo hayo na pia kupanga mpango kazi mkakati utakaowasaidia kutekeleza kazi hiyo baada ya mafunzo kukamilika.

 

Upande wake Afisa Utumishi Peter Kafuku amesema Mafunzo hayo yatakapokamilika yatawasaidia wafanyakazi ambao ndio watoa huduma kwa Wananchi kutambua viashiria mbalimbali vinavyoweza kusababisha hatari katika utendaji wa kazi vinavyoweza kujitokeza katika Mazingira na sura mbalimbali. Wakiweza kutambua viashiria Hivyo itakua rahisi kuviepuka, kukabiliana navyo na kutoa huduma ipasayo kwa Wananchi.