Mazingira FM

Bunda: wakazi wa Bunda stoo wilayani Bunda wawapongeza viongozi kwa ujenzi wa kivuko (daraja)

2 December 2022, 12:44 pm

Wakazi wa Mgayangobo mtaa wa Miembeni kata ya Bunda Stoo mjini Bunda wamewashukuru viongozi wa kata hiyo kwa kutatua changamoto ya kivuko katika eneo hilo
Wakizungumza na Mazingira Fm wakazi hao wamesema imekuwa changamoto kubwa wakati wa kuvuka hasa kwa watoto kipindi cha mvua.

Aidha wameongeza kuwa wanawashukuru mbunge wa Bunda Mjini Robert Mabotto kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo Flaviani Chacha kwa kuona umuhimu wa daraja hilo.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Bunda Stoo Flavian Chacha amesema daraja hilo limejengwa kwa ushirikiano kati yake kama diwani mbunge wa jimbo la Bunda mjini na wakazi wa eneo hilo.


aidha ameongeza kuwa iku za hivi karibuni wataanza kuchonnga baadhi ya barabara katika kata hiyo ikiwemo ya kwa manguruwe.