Mazingira FM

Tatizo la Maji Safi na salama Bado changamoto Chuo Cha Kisangwa FDC

25 November 2022, 6:56 pm

 

 

Tatizo la Maji Safi na salama imetajwa kuwa bado changamoto katika Chuo Cha maendeleo ya wananchi Kisangwa FDC

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo hicho Edmundi Nzowa katika mahafali ya 36 ya Chuo hicho ambapo jumla ya wahitimu 137 katika fani mbalimbali kama vile Kilimo na Mifugo, Ufundi umeme, uselemara miongoni mwa Fani zingine.

Nzowa amesema tatizo la Maji limekuwa changamoto ya muda mrefu katika Chuo hicho huku kipindi Cha kiangazi wanafunzi ulazimika kutumia maji ya kwenye madimbwi ambayo si salama kwa Afya za wanafunzi hao

Aidha Nzowa amesema kutokana na hamasa ya wazazi kuwaleta wanafunzi chuoni hapo kwa sasa miundombinu iliyopo haitoshi kama vile mabweni, vyumba vya Madarasa na upungufu wa watumishi

Nzowa ameongeza kuwa kwa sasa Chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 310 kwa mwaka 2022 ukilinganisha na wanafunzi 288 kwa mwaka 2021

Akizungumza katika mahafali hayo Mary Machogu kwa niaba ya mgeni rasmi amesema changamoto mbalimbali zilizoainishwa katika risala ya wanafunzi na shule anazichukua na kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na ofisi ya mbunge Jimbo la Bunda mjini waone namna ya kutatua changamoto hizo

Aidha amewataka wanafunzi hao kudumu katika maadili mazuri ili waepuke changamoto za ukosefu wa ajira kutokana na ukosefu wa nidhamu