Mazingira FM

Bunda; Rasmi Serikali yatangaza kuwaamisha wakazi wa kata Nyatwali kupisha mbuga ya Sarengeti

November 17, 2022, 9:36 pm

Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa uamzi rasmi wa kulitwaa eneo la kata ya Nyatwali kwa matumizi ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Uamuzi huo umetolewa na katibu tawala  wilaya ya Bunda Salumu Mtelela katika mkutano wa baraza la madiwani hamashauri ya mji wa Bunda kwenye kiko cha kawaida cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 ambapo amesema kuwa serikali  imetoa walaka wa kuchukuliwa eneo la nyatwali  na kusitisha shughuli zote ambazo zinaendelea na kuwa hifadhi ya taifa ya Serengeti .

kauli hiyo ameitoa baada ya diwani wa kata hiyo Malongo Mashimo kuibua hoja ya ujenzi wa miradi ya Maendeleo ya barabara katika kata hiyo .

Mterela amesema kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa na Serikli  kwaajili ya kulinda ekolojia ya hifadhi ya taifa ya Serengeti  na kuwalinda wananchi ambao wamekuwa wakilalamika mara kwa  mara kuvamiwa na wanyama waharibifu .

Hata hivyo Mtelela amesema   uamuzi huo na mpango wa kutwaa eneo la nyatwali umekamilika tarehe 11 November katika kikao  kilichoongozwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suluhu hasani.