Mazingira FM

Bunda; mwanafunzi kidato cha pili apoteza maisha baada ya kushambuliwa na mamba ziwani

11 November 2022, 9:13 am

 

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Yusuph Yohana Marwa umri miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Guta na mkazi wa mtaa wa nyabehu kata ya Guta halmashauri ya Mji wa Bunda amepoteza maisha baada ya kushambuliwa na mamba wakati akioga kandokando ya ziwa Victoria

akizungumza na radio mazingira Fm mwenyekiti wa mtaa wa Nyabehu Richard Makanga amesema tukio hilo limetokea majira ya saa nne Asubuhi 9 Nov 2022 wakati Yusuph na wenzake walioenda kuoga ziwani kama yalivyo mazoea yao

 

Aidha richard amesema kwa sasa mamba wamekuwa wengi katika eneo hilo hivyo anaomba serikali kuchukua jitihada za kuwavuna ili kuokoa maisha ya wananchi kwa kuwa hili ni tukio la tatu