Mazingira FM

Wenyeviti wa vijiji Bunda Wapewa somo kuhamasisha chanjo ya UVIKO -19

22 October 2022, 8:33 pm

 

 

Katibu tawala wilaya ya bunda salumu halfan mterela amewataka viongozi wa vijiji na mitaa kuhamasisha wananchi kujitokeza katika kampeni ya siku kumi ya kuhamasisha chanjo ya uviko 19

 

Akizungumza katika kikao kilichoshirikisha idara ya afya na wenyeviti wa serikali za vijiji kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda mh mterela amesema viongozi wanao wajibu wa kuhamasisha wananchi kuchanja chanjo ya korona kwa kuwa ugonjwa huo bado upo  na halmashauri nya wilaya ya Bunda imechanja asilimia 34 tu

Kwa upande wao wenyeviti  wamesema zipo changamoto  za kutoshirikishwa katika kazi mbalimbali zinazotekelezwa katika maeneo yao hivyo  ni vema wawe wanashirikishwa kwa kuwa ndiyo wanakaa na wananchi