Mazingira FM

SIKIKA TAKUKURU, zaendesha mafunzo kutokomeza rushwa kwenye huduma za afya

October 22, 2022, 8:28 pm

Sikika kwa kushirikiana TAKUKURU wilayani Bunda wameendesha mafunzo kwa kamati za ujenzi na mapokezi kwa lengo la kuzuia masuala ya rushwa wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Mafunzo hayo yamefanyika wilayani Bunda ambapo Sikika kwa  kushirikiana na TAKUKURU chini ya mpango wa ufadhili wa shirika la maendeleo vijijini UNDP wanalenga kutokomeza mianya ya rushwa kwenye huduma za afya.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo HANGTON MUGABE mjumbe wa kamati ya ujenzi na mtendaji kata ya Nyamuswa amesema mafunzo haya yatakuwa tija kwa kamati zote kwa kuwa kila mjumbe atatekeleza wajibu wake kwa kufuata utaratibu tofauti na awali walivyokuwa wakitumia uzoefu