Mazingira FM

Shule ya balili mjini Bunda yakabiliana na upungufu wa matundu ya vyoo 28

22 October 2022, 8:24 pm

 

Imeelezwa kuwa upungufu wa matundu 28 ya vyoo shule ya msingi baliliĀ  A bado limekuwa changamoto katika shule hiyo.

Hayo yamebainishwa katika risala ya wanafunzi wa darasa la saba katika mahafari yao ya kuhitimu elimu ya msingi yaliyofanyika leo .

Kwa niaba ya mgeni rasmi FRANK MAMBA amesema amesikitika kwa shule kongwe kama balili kukosa choo hivyo ametoa tofari 300 na mifuko mitano ya saruji ili iweze kuwa mwanzo wa shule hiyo kujenga choo kwa ajiri ya shule hiyo

Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi balili WILIESA MAKORI NGEA amesema changamoto zipo nyingi katika shule ya balili ikiwemo vyoo kwa walimu na wanafunzi, nyumba za walimu huku akiiomba serikali kusaidia katika kutatua changamoto za shule hiyo