Mazingira FM

Salumu Mterela DAS Bunda; afunga maadhimisho ya elimu ya watu wazima Bunda

22 October 2022, 8:09 pm

it

katibu tawala wa wilaya ya Bunda mh. Salum Mtelela amesema  ofisi ya mkuu  wa wilaya ya Bunda itaongeza bajeti ya elimu ya watu wazima ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wengi wanajiumga na elimu hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya wakati akijibu risala iliyosomwa na mkurugenzi wa chuo cha The Golden city collage Lucas Gabriel  Katibu tawala wa wilaya ya Bunda mh. Salum Mtelela amesema mbali nakuongeza bajeti pia wataendelea kutoa elimu kwa kutumia vyombo vya habari kuondoa dhana potofu juu ya elimu ya watu wazima.

Aidha Mh. Mtelela ameongeza kuwa suala la ucheleweshwaji wa vyeti kwa wahitimu kwa vyuo vya elimu ya watu wazima wao kama viongozi watalishughulikia ili viweze kutoka kwa wakati.

Katika hatua nyingine wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wanaofundisha elimu hiyo na wanafunzi  wanaosoma elimu hiyo wamesema changamoto wanazozipata ni umbali kwasababu shule ya Kabasa ndo shule pekee ambayo imeteuliwa kufundisha Elimu hiyo maalum