Mazingira FM

BUNDA. Wananchi wahimizwa kununua mahindi ya bei nafuu yaliyoletwa na serikali

22 October 2022, 8:14 pm

Katibu tawala wilaya wilaya ya bunda salum mterela amewahimiza wananchi wa wilaya ya bunda kutumia fullsa ya mahindi ya bei nafuu yaliyoletwa na serikali wilayani bunda.

Mterela ameto msisitizo huo leo ofisini kwakwe wakati akiongea na vyombo vya habari ambapo amesema kwa sasa mahindi yanapatikana katika halmashauri zote mbili za wilaya ya bunda huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kununua mahindi hayo ambayo kwa halmashauri ya wilaya vituo ni mugeta na nyamuswa huku upande wa halmashauri ya mji kituo ni bunda stoo eneo la miembeni

Aidha mh mterela ametoa onyo kwa wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi wa mahindi hayo kwa minajili ya kwenda kuuza kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na hatua zitachukuliwa