Mazingira FM

Diwani wa Ketare, Mramba Simba aahidi kutatua changamoto katika shule ya sekondari Esperanto

14 October 2022, 5:23 pm

 

Diwani wa kata ya Ketare  halmashauri ya  wilaya ya Bunda mkoani Mara ndugu Mramba Simba Nyamkinda  ameahidi kutekeleza changamoto mbalimbali zilizopo katika shule ya sekondari Esperanto.

Akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya kidato cha nne ya shule hiyo baada ya kupokea changamoto mbalimbali zilizosomwa katika risala iliyowasilishwa na wanafunzi na uongozi wa shule, Mramba amesema kati ya changamoto 6 zilizowasilishwa katika mahafali yaliyopita tayari ametekeleza changamoto 5

Katika hatua nyingine Mramba Simba ameahidi kuongeza urefu wa kisima cha maji, kuweka tangi la lita laki 2.5 kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua na kuweka mfumo wa Internet utakaowawezesha wanafunzi na walimu kujifunza kwa mfumo wa TEHAMA huku akitoa televisheni nchi 43 katika shule hiyo kwa matumizi ya mfumo wa kimasomo.