Mazingira FM

Diwani wa kata ya ketare atimiza ahadi kwa wanafunzi 19 wa shule ya msingi ketare waliofanya vizuri kwenye mtihani

14 October 2022, 5:19 pm

 

Diwani wa kata ya Ketare ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara Mhe Mramba Simba Nyamkinda  amekabidhi vifaa vya shule mbalimbali vya shule kwa wanafunzi 19 wa shule ya msingi Ketare waliofanya vizuri katika mitihani ya nusu muhula mwaka huu.

Akizungumza katika kukabidhi zawadi hizo mapema leo  12 oct 2022 Mhe Mramba amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na zawadi hizo ziwe chachu ya wao kuendelea kuweka bidii katika masomo yao

Miongoni mwa vifaa alivyotoa kwa wanafunzi hao ni pamoja na sare za shule ikiwa ni shati, kaptula au sketi, viatu , soksi , daftari , kalamu, pamoja na mfukon wa kubebea daftari

Sambamba na hilo pia Mhe diwani ametoa meza na na viti kwa shule za msingi Ketale na shule shikizi ya Nyakongo kwa ajili ya matumizi ya walimu.