Mazingira FM

DAS Bunda, marufuku uongozi wa machinga kutoza faini

October 14, 2022, 5:04 pm

Katibu Tawala Wilaya ya Bunda Moani Mara, Salumu Mtelela amepiga marufuku umoja wa Machinga kutoza faini wala kutoza ushuru katika masuala yanayohusu usafi wa Mazingira.

Kauli hiyo ya Mtelela imekuja baada ya kupokea kero na malalamiko mbalimbali ya wafanyabiashara na wajasiriamali katika wa kikao cha kusikiliza  kero na changamoto kilichofanyika maeneo ya stendi mpya mjini Bunda jana tarehe 12 Oct 2022 ambapo pamoja na mambo mengine wamelalamika kutozwa faini na ushuru pasipo utaratibu maalumu.

Katika hatua Nyingine imesisitizwa kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali hawatakiwi kufanyia Biashara katika eneo hilo kwa siku za Jumanne kama ilivyoelekezwa tangu awali