Mazingira FM

DAS Bunda: awataka wanafunzi kuacha kujihusisha na mahusihano ya kimapenzi badala yake wajikite kwenye masoma

14 October 2022, 4:53 pm

Wito umetolewa kwa wanafunzi kujiepusha na masuala ya mahusiano ya kimapenzi angali wakiwa shuleni badala yake wajikite kwenye kusoma

Hayo yamesemwa na katibu tawala wa Wilaya ya Bunda Mhe Salum Alfani Mterela wakati wa Ziara yake ambapo amezungumza na wanafunzi wa kike shule ya Sekondari Rubana na ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanafunzi wa kidato Cha pili na nne kufanya maandalizi kwa ajili ya mitihani ya taifa

Aidha ameongeza kwa kuwasisitiza  wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutengeneza nafasi za kuwa viongozi wa baadae ikiwa jambo ambalo halikutegemewa saizi Rais wa Tanzania ni mwanamke ambaye ni Mhe Samia Suluhu Hassan