Mazingira FM

Wangonjwa 90 wa macho wafanyiwa upasuaji kwenye kambi ya matibabu

25 September 2022, 8:58 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassar amezindua kambi ya matibabu kwa wangojwa katika hospitali ya wilaya ya Bunda Manyamanyama inayodhaminiwa na kamati ya kukuza na kuendeleza uislamu Tanzania

 

Akizungummza katika uzinduzi huo mhe mkuu wa wilaya ameishukuru kamati ya kuendeleza uislamu nkwa kujitolea kughalamikia matibabu kwa wagonjwa kwa kuwa hata maandiko matakatifu yanasema dini iliyosafi ni ile inayohudumia wajane, yatima na wasiyojiweza

 

Kwa upande wake amiri wa kamati ya kuendeleza uislamu wilaya ya Bunda Saidi Sumanne Kizigo amesema anawashukuru viongozi kwa kushirikiana na kamati hiyo kuakikisha kambi hii inafanikiwa kwa hadi kufika leo zaidi ya wagonjwa 200 wamefika kupimwa huku wagonjwa wapatao 90 wamefanyiwa upasuaji wa macho

Awali akizungumza mbele ya mgeni rasmi katibu wa kamati ya kuendeleza uislamu mkoa wa Mara Dkt Makame Maulidi amesema changamoto inayoikabili kamati hiyo kwenye kambi ni wingi wa wangonjwa ukilinganisha na makisio, ufinyu wa bajeti miongoni mwa changamoto zingine.