Mazingira FM

baraza la madiwani bunda mjini lafanya kikao chake cha robo ya nne ya mwaka huku Dampo na sehemu ya maziko vikichukua nafasi

9 September 2022, 12:39 pm

Baraza la madiwani halmashauli ya mji wa bunda limefanya kikao chake cha robo ya nne ya mwaka mbapo madiwani wameitaka halmashauri kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo na kiwango cha fedha kinachotumika kutekeleza miradi hiyo

Wakizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri bunda mjini  waheshimiwa madiwani miongoni mwa hoja walizobainisha ni pamoja na dampo  na sehemu ya maziko katika eneo la migungani ambapo wamebainisha eneo hilo watu kuendelea kujenga karibu nalo

Kwaupande  mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa bunda Emmanuel Mkongo amewataka madiwani kushirikiana na wataalamu wa halmashauri kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao huku akibainisha kazi yake ndani ya bunda ni kuwa mkurugenzi na si vinginevyo

Naye mkuu wa wilaya ya bunda mh Joshua Nassar akitoa salamu za serikali amewapongeza   madiwani na halmashauri ya mji wa Bunda kwa kushika nafasi ya 7 kati ya halmashauri 184  na kuiheshimisha wilaya