Mazingira FM

Bunda: Gurumet yatoa Elimu kwa vijiji vilivyopo karibu na hifadhi ya Serengeti kujilinda na wanyama waaribifu

July 22, 2022, 6:17 am

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mheshimiwa Joshua Nassari amehitimisha zoezi la utoaji Elimu kuhusu kukabiliana na wanyamapori wakali pamoja na waharibifu kwa wakazi wanaozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Ili kuepuka na kupunguza madhara yanayotokana wanyama hao.

 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Guta halmashauri ya mji wa Bunda Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Nassar amewataka wakazi wa maeneo yote yanayozunguka Hifadhi ya Serengeti kutumia vyema mafunzo waliyoyapata Katika kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mbinu walichofundishwa za kukabiliana na wanyama wakali.

Naye mhifadhi mkuu kutoka Ofisi ya TAWA Kanda ya Ziwa John Msirikale amesema mapokeo yamekuwa makubwa kwa wananchi juu ya Elimu hiyo huku akiwapongeza wananchi ambao wameshiriki vyema Katika Zoezi hilo.

Aidha Msirikale amesema wametoa Elimu pamoja na kuwapatia vifaa mbalimbali vya kukabiliana na wanyama hao kama vile vilipuzi, pilipili, tochi na vifaa vingine vitakavyowasaidia.

Kwa upande Meneja Mahusiano wa Grumeti fund David Mwakipesile ameeleza kuwa mara baada ya kupokea mualiko kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na kutokana na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza katika vijiji na Mitaa vinavyozunguka Hifadhi, Shirika la Grumeti liliamua kushiriki Moja kwa Moja kudhamini mafunzo haya Ili kupunguza vifo na uharibifu wa mazao.

Jumla ya vijiji Tisa vya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambavyo ni Tingirima, Kiandege, Sarakwa, Mariwanda, Kihumbu, Hunyari, Buzimbwe na Kabainja huku Mitaa 13 ya Halmashauri ya Mji wa Bunda ambayo ni Mihale, Kiharagweta, Nyamatoke, Bukore, Mitimirefu, Ichamu, Kunzugu, Balili, Rubana, Butakale na Mitaa yote ya Guta imefikiwa na elimu hiyo.

#grumetfund
#wanyamapori
#tawa