Mazingira FM

Hapi: awaomba wazee Mara kusaidia kuondoa ubinafsi kwenye jamii

June 22, 2022, 7:47 am

 

Mkuu wa Mkoa wa Mara amewaomba wazee wa mkoa huo kusaidia kukemea ubinafsi ambao unapelekea kuwepo hali duni za maendeleo unasababishwa na baadhi ya wananchi na viongozi kukwamisha baadhi ya miradi inayoletwa na Serikali.

Kauli hiyo ametoa wakati akizungumza na Wazee wa kimira,wazee wa baraza,wazee wastaafu, Wazee wa Chama na machifu kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa uwekezaji wa mkoa huo.

amesema serikali imekuwa ikileta miradi mbalimbali lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakikwamisha kutokana na sababu zao wanazozijua huku akitoa mifano mbalimbali ya miradi iliyokwamisha kabla ya serikali kutumia nguvu katika utekelezaji wa miradi hiyo katika wilaya ya Rorya.

Hapi amesema kutokana na ubinafsi huo kumesababisha viwanda kuendelea kufa hali inayochelewesha maendeleo wakati rasilimali nyingi ukiwemo ufuke mzuri na ulimaji wa mazao ya kahawa na pamba unashamili vizuri mkoa huo.

Amewataka pia kufuatilia fedha inazoletwa na serikali kwenye miradi ambapo amewapongeza wazee kukomesha baadhi matukio yanasababisha uharibifu katika mkoa huo ambapo kwa sasa ni shwari kwa usalama tofauti na hapo nyuma na kutaka kuendelea kudumisha amani.

Katika hatua nyingine amewataka Waganga wakuu kuhakikusha dawa za kutosha zinakuwepo kwa ajili ya matibababu sambamba na kuwapa vitambulisho ili viwasaidie kupata matibabu kwa haraka.

Kupitia kikao hicho Mkuu wa Wilaya Rorya Juma Chikoka akapewa massa 48 na Mkuu wa Mkoa kuhakikisha Mganga wa afya wa zahanati ya Oliyo pamoja na kuweka ulinzi mkali kufuatia wananchi wa eneo hilo kugoma kutumika kwa zahanati hiyo kwa madainkiwa wao walihitaji kituo cha afya na sio zahanati.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka amesema kwa sasa wananchi watakaogoma kwenda kupewa huduma ya afya katika zahanati hiyo watachukuliwa hatua Kali za kisheria maana Serikali imewekeza hela nyingi kwa ajili ya kuwasadia wananchi waondokane na changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuatia huduma ya afya.

Kwa upande wao wazee wa Mila wamesikitika kusikia kwenye kikao hicho kuwa wananchi wamegoma kupata huduma ya afya katika zahanati hiyo ,kwani kama Serikali ingewashirikisha basi kusingekuwepo na shida yoyote.