Mazingira FM

NBS: 85% ya wananchi wameshaanza kuwa na uelewa wa zoezi la sensa

June 17, 2022, 12:44 pm

Saidi Amiri Afisa Habari kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu

Kwa mujibu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu 85% ya wananchi tayari waishaanza kuwa na uelewa kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Hayo yamesemwa Leo June 17, 2022 Mkoani Iringa na SAID AMIRI ambaye ni Afisa Habari kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS ambapo amesema elimu itasaidia wananchi kujiamini na kuweza kutoa taarifa ambazo ni sahihi wakati wa kuhesabiwa

Imetajwa kuwa upo umuhimu mkubwa wa elimu ya sensa na uhamasishaji wa jamii katika kipindi hiki Cha sensa ya watu na makazi

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania wakifuatilia wawezeshaji katika mafunzo juu ya sensa ya watu mwaka 2022 . Mkoni Iringa

Aidha Saidi ameongeza kuwa wamelenga kutoa elimu kwa wananchi ili zoezi la sensa lifanyike bila vikwazo, kuwaleta karibu wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile viongozi wa Dini

Ameongeza kuwa utoaji wa elimu unasaidia kumpunguzia kalani wa sensa kazi wakati wa sensa, kumfanya mwananchi kujiamini wakati wa kuhesabiwa kwa kuwa Taarifa zote anazo na inasaidia uokoaji wa muda katika kipindi Cha kuhesabu watu.

#sensakwamaendeleojiandaekuesabiwa2022

#Tadio

#wizarayaardhi

#wizarayahabari

By Adelinus Banenwa