Mazingira FM

apoteza maisha akitajwa kufukiwa na kifusi kwenye machimbo ya kokoto :Bunda

26 April 2022, 7:24 pm

Machimbo ya kokoto  Manyamanyama

Mwanamume mmoja aliyetambulika kwa jina la James Mathias 40 mkazi wa Manyamanyama Halmashauri ya Mji wa Bunda amepoteza Maisha akitajwa kufukiwa na kifusi wakati akichimba kokoto kwenye machimbo ya kokoto Manyamanyama.

Wakizungumza na Mazingira Fm mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea Leo 26 April 2022 majira ya saa saba mchana wakati wakiwa wanaendelea kuchimba ndipo kifusi  kilishuka na kumfukia mwenzao.

.

Mwenyekitiwa mtaa wa katoliki Juma Ipalapala Sindano amesema baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio la mtu kufukiwa na kifusi alifika machimboni hapo na kuwapigia simu polisi ambao walifika na baada ya vipimo  waliamuru mwili upelekwe mochwari.

.

Kwa upande wa mke wa marehemu amesema amepata taarifa majira ya saa Saba mchana alipofika akakuta anafukuliwa kutoka kwenye kifusi.

James Mathias ameacha mke na watoto wanne

Juhudi zinaendelea kuwatafuta jeshi la police kwa taarifa zaidi