Mazingira FM

Mtangazaji wa Mazingira fm Tedy Thomas: atangazwa mwanamke shujaa Mkoa wa Mara kwa kupinga ukatili wa kijinsian

9 March 2022, 6:57 am

Tedy Thomas mtangazaji wa Redio Mazingira fm akiwa kwenye mkutano wa kimataifa wa kupinga unyanyasaji wa kijinsia nchini Afrika ya Kusini

Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake Duniani nchini Tanzania pia ni miongoni mwa mataifa yaliyoungana na Dunia kusherekea siku hii muhimu kwa kauli Mbiu isemayo *@Haki na usawa kwa maendeleo endelevu. Jitokeze kuhesabiwa#*

Mkoani Mara Mwandishi wa Habari na mtangazaji wa kituo Cha Redio Mazingira fm iliyopo Bunda *Tedy Thomas Kiyombi* ametangazwa kwenye maadhimisho ya kimkoa kama mwanamke shujaa wa Mkoa wa Mara kwa habari zake za kutetea usawa wa kijinsia na kupinga ukatili kwa wanawake na mafanikio aliyoyapata kitaifa na kimataifa kwa kazi hiyo.

Tedy Thomas kushoto akitangazwa kama mwanamke shujaa Mkoa wa Mara kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

Maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Mara yamefanyika Wilayani Butiama ambapo yamewakutanisha wanawake wote wa Mkoa wa Mara katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

Kwaniaba ya uongozi wa Redio Mazingira FM tunakupongeza Tedy Thomas Kiyombi kwa kutunukiwa heshima hii Hongera Sana