Mazingira FM

Mh.Nassar: Azindua zoezi la Anwani za makazi Wilaya ya Bunda

9 March 2022, 8:52 pm

Mh Joshua Nassar mkuu wa Wilaya ya Bunda akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Bunda katika uzinduzi wa Anwani za makazi

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar amezindua rasmi zoezi la uwekaji wa anuani za makazi

Hafla hiyo imefanyika viwanja vya stendi ya zamani Bunda mjini Leo march 9, 2022

Akizungumza kwenye uzinduzi huo mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh Joshua Nassar amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa mitaa na Vijiji kuchangia gharama za vibao vinavyoainisha majina ya mitaa hiyo kwa kuwa gharama hizo ni jukumu la wananchi kwa maelekezo ya serikali

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Anwani za makazi Wilaya ya Bunda

Hata hivyo Mh Nassar amebainisha Faida zilizopo kwenye zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na kwa maeneo yote kupitia kanzi data

Pia mh Nassar ametumia mkutano huo kuendelea kuwaamasisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule waliofaulu kuingia kidato Cha kwanza ambapo amebainisha kuwa zaidi ya watoto elfu Moja kwenye Halmashauri zote mbili hadi sasa hawajaripoti shuleni hivyo ametoa wiki Moja kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu wanaripoti baada ya hapo kwa wazazi watakaokaidi hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

Vile vile mkuu wa Wilaya aligusia suala la usafi wa Mazingira ambapo amewataka viongozi ngazi ya kata na Vijiji kuhakikisha wanalinda Mazingira na kuhimiza watu kuacha ukataji wa mkaa ili kuyalinda Mazingira