Mazingira FM

UWT Bunda: watembelea hospital ya Manyamanyama kuwasalimia wanawake waliojifungua

8 March 2022, 9:36 am

UWT Bunda wakiwa na muuguzi mkuu wodi ya wazazi hospital ya Manyamanyama kuelekea siku ya wanawake duniani

Kuelekea siku ya kilele Cha maadhimisho siku ya wanawake duniani march 8 jumuiya ya UWT wilaya ya Bunda na kamati ya utekelezaji chama Cha Mapinduzi wametembelea hospital ya Manyamanyama iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bunda ili kuwaona wanawake waliojifungua katika hospital hiyo.

kupitia kwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Bunda Mama Sabuni amesema pamoja na huduma nzuri inayotolewa lakini hospital hiyo bado haijapewa kipaumbele ikiwemo majengo vifaa tiba wataamu kwa kuwa inahudumia watu wengi

Mama Sabuni mwenyekiti UWT Akimpongeza mama aliyejifungu

Mwenyekiti wa UWT ameitaka serikali ya Wilaya ya Bunda kuipa hadhi ya hospital ya Manyamanyama kuwa hospital ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kuwa eneo linatosha

“Kuna taarifa kwamba Halmashauri ya Mji wa Bunda unatafuta eneo la kujenga hospital ya Halmashauri tunatafutaje eneo lingine wakati tayari ndani ya hii Halmashauri kuna hospital ambayo pia imeshapewa hadhi ya Halmashauri kupitia Wizara ya Afya barua iliyotolewa na katibu mkuu Wizara ya Afya mwezi Feb 2021 sasa hiyo iliishia wapi?”

Pamoja na mambo mengine uongozi wa hospital ya Manyamanyama wametoa Rai kwa wanawake wote kuudhuria clinic kipindi Cha ujauzito na kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kama vituo vya Afya na hospital ili kulinda Maisha ya mama na mtoto