Mazingira FM

Serengeti: kesi ya babu wawili waliobaka mjukuu kwa zamu mmoja akutwa na Hatia

March 7, 2022, 7:35 pm

HUKUMU YA KESI YA BABU WAWILI WALIOBAKA MJUKUU KWA ZAMU MMOJA AKUTWA NA HATIA

SERENGETI.Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imemhukumu Hamisi Maganga(50) mkazi wa kijiji cha Natta kutumikia kifungo cha miaka 30 na faini ya Sh1milioni kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 12,huku Magembe Magangila(50) akiachiliwa huru.

Akisoma hukumu katika kesi ya jinai namba 1/2022 leo Jumatatu Machi 7 Hakimu Mkazi wa Wilaya Adelina Mzalifu amesema,mshitakiwa huyo amehukumiwa adhabu hiyo kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ukihusisha watu wanne na haukuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo.

Amesema kwa upandewa Magangila ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulikuwa wa kimazingira zaidi haukuweza kuthibitisha kama alitenda kosa,hasa Polisi wa Kituo cha Natta ambaye alisema walilazimika kumweka ndani kwa usalama wake baada ya watu kudai alihusika,wakati yeye alishiriki kumkamata mtuhumiwa kwa tuhuma za kumbaka huyo mtoto.

Na katika Utetezi wake Mahakamani alisema siku ya tukio hakuwepo na alileta shahidi ambaye aliithibitishia mahakama kuwa hakuwepo huku Hamisi akishindwa kujitetea kwa madai kuwa anaiachia Mahakama iamue.

Alipopewa nafasi ya kujitetea baada ya kutiwa hatiani Maganga ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye ni baba wa familia ana mke na watoto wanamtegemea.

Desemba 17 kati ya saa 5.30 na saa 6.00 usiku katika Kitongoji cha Majengo nyumbani kwa Dorika Kambarage bibi wa mtoto huyo watuhumiwa Magembe Magangila mme wa bibi huyo na Hamisi Maganga mme wa shangazi ya mama wa mtoto wanadaiwa kumbaka kwa zamu huku wakitishia kumuua iwapo angesema.

Katika tukio hilo mtoto huyo aliumizwa na kulazimika kulazwa Kituo cha Afyacha Natta kwa siku tano,alishonwa na kuongezewa damu