Mazingira FM

Tembo waua tena wawili na kujeruhi mmoja Bunda

February 3, 2022, 8:17 am

Watu wawili wamepoteza maisha na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na tembo wakati wakijaribu kuwafukuza tembo waliokuwa wamevamia makazi ya watu katika mtaa wa Bushigwamala kata ya Guta, Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Makongeni kata ya Tairo Halmashauri ya mji wa Bunda, Marwa Mwita amesema katika tukio hilo lililotokea jana majira ya jioni wananchi wakiwa katika jitihada za kuwafukuza Tembo waliovamia makazi hayo ghafla Tembo mmoja aligeuka na kuanza kuwakimbiza ambapo watu wawili walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na tembo.

Waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Elias Kaisamu Wambura mkazi wa Bushigwamala na John Kambarage Wambura miaka 22 mkazi wa Rwamkoma-Butiama ambaye alifika Bushigwamala tangu siku ya jumamosi kumtembelea shemeji yake na majeruhi ni Juma Alfred miaka 20 mkazi wa Makongeni

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda na ndugu wa marehemu hao wasema:

Joram Kambona ni Daktari katika hospitali ya DDH Bunda amethibitisha kupokea miili ya watu hao

By Edward Lukas