Mazingira FM

Tembo waharibu Ekari 50 za mahindi na mtama

January 29, 2022, 6:48 pm

baadhi ya mashamba yaliyoliwa na Tembo

Takribani ekari 50 za mahindi na 10 za pamba kata ya bunda stoo halmashauri ya mji wa bunda zimeliwa na tembo usiku wa kuamkia tarehe 28 jan 2022

Hayo yamesemwa na Afisa kilimo wa kata ya Bunda stoo Mboji Shibole Kulwa wakati akizungumza na Mazingira Fm katika eneo la mashamba yaliyoko  eneo la Bigutu mtaa wa idara ya maji alipofika kuwafanyia tathmini wakulima walioathirika na wanyama hao

Kwa upande wa  wakulima wameelezea kero ya tembo kuwa jambo lililowatesa na hadi sasa serikali haijalipatia ufumbuzi ambapo kwa sasa tembo wamekuwa wengi hata vyakula vilivyokuwa haviliwi na tembo zamani  sasa  wanakula

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Idara ya maji ndugu Mtaki Bwile  amesema changamoto ya tembo katika mtaa wa idara ya maji kata ya Bunda stoo imekuwa ya kujirudiarudia sana jambo linaloleta mashaka hata kwa wakulima kuendelea nakilimo katika maeneo hayo maan wali wengi wanakopa pembejeo na mashamaba yao niyakukodi

by Adelinus Banenwa