Mazingira FM

Bunda: Nyumba tatu zabomolewa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi

26 January 2022, 7:55 am

Nyumba tatu (slop) za mzee Paul Muhere Maneno mkazi wa mtaa wa Kilimahewa Kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara zimebomolewa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumzia na Redio Mazingira fm,mtendaji wa Kata ya Kabarimu Ndugu William Magebo amesema.
“Wananchi wamebomoa nyumba tatu za mzee Paul Muhere Maneno January 24 mwaka huu na siku ya leo wananchi hao hao wakaamua kuchoma Mali za mzee huyo kwa tuhuma za wizi wa kijana wake”

Magebo amesema chanzo cha tukio hilo ni tuhuma za wizi ambapo kijana wa mzee huyo Yusuph Paul Muhere (16) anatuhumiwa kuwa ni mwizi na wananchi wa eneo hilo.
Hadi sasa familia ya mzee huyo imekimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wao.

kwa upande wake Paul Muhere Ambaye ndiye mmiliki wa Nyumba hizo amesema hadi sasa anahofia usalama wake na familia tayari ameiondoa kwenye Mazingira hayo na kudai kijana anayelalamikiwa ambaye ni Yusuph haishi kwake iweje wabomoe Nyumba zake? Na amesema tayari ameshachukua RB kituo Cha Polisi Bunda lakini bado Hana Imani na usalama wake.